Home » » SIMBAALIA ATAKA TANESCO KUACHA URASIMU

SIMBAALIA ATAKA TANESCO KUACHA URASIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha wananchi wanaokwenda kuomba huduma ya kuunganishiwa umeme wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati.
Simbakalia alitoa rai hiyo mjini hapa jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa  viongozi wa Tanesco uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi (VETA) mkoani hapa.
“Nimeambia moja ya ajenda zenu ni kujadili namna bora ya kufanya mabadiliko ya ndani ili kufanya Tanesco kuwa shirika bira, ni vema mkaanzia mkakati ambao utakuwa endelevu wa kufanyakazi nje ya mazoea na kila mfanyakazi alitambue hilo na wateja wenu waone kuna tofauti,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema katika mkutano huo watajadili utekelezaji na maendeleo ya shirika pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanatoa huduma bora ya kumthamini mteja.
“Tunataka kuhakikisha wafanyakazi wote wa Tanesco wanatoa huduma bora kwa wateja na kumpa huduma anayostahili,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa