Home » » Kampuni yatozwa bil. 1/- kwa uzembe

Kampuni yatozwa bil. 1/- kwa uzembe

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KAMPUNI ya ujenzi ya Db Shapriya Co  LTD, imepewa adhabu ya kulipa sh milioni 11 kila siku  kwa siku 100 kuanzia Machi 4, mwaka huu, kutokana na kutomaliza mradi wa ujenzi wa  barabara kwa wakati.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, alipozungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani, baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo imefadhiriwa na Benki ya Dunia.
“Kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu kucheleweshwa kwa kukamilika kwa wakati kwa barabara  ambazo zinatengenezwa  na Kampuni ya Db Shapriya leo niliamua kukagua miradi ya maendeleo  iliyopo maeneo ya Mangamba, Sabodo, Soko Kuu na Barabara ya Chuno, Barabara ya Kunambi pamoja na kutembelea eneo linapojengwa dampo la kisasa  lililopo Mangamba na kukagua vizimba vyake 25.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa