Home » » MTWARA WATAKIWA KULIMA MAZAO MBADALA

MTWARA WATAKIWA KULIMA MAZAO MBADALA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WANANCHI mkoani Mtwara wamehimizwa kulima mazao mbadala ya biashara na sio kutegemea kilimo cha korosho pekee.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, katika mkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, kuhusu utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari 2012 hadi Desemba,  mwaka jana, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini hapa.
Ndile alisema ni vizuri wananchi wakatambua kulima mazao mbadala ya biashara, ili kujiongezea kipato ndani ya familia zao na sio kutegemea zao moja la biashara.
 Chanzo:Taanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa