Home » » BREAKING NUUUZ: WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA VURUGU ZA WANANCHI NA POLISI MTWARA.

BREAKING NUUUZ: WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA VURUGU ZA WANANCHI NA POLISI MTWARA.

Mtwara,Tanzania
WATU watatu wamefariki Dunia katika mapambano ya Askari Polisi na Wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyosomwa leo na Waziri Profesa Sospeter Muhongo.

Mbali na watu hao kuuawa Askari mmoja wa Jeshi la Polisi pia amejeruhiwa vibaya baada ya kucho
mwa mshare katika mapambano hayo yaliyoanza saa 12 asubuhi,katika maaeneo mbalimbali yaliyokuwa yametekwa na waandamanaji hao.

Mwandishi wa Habarimpya.com aliyekuwa katika maeneo ya Mikindani anaripoti kwamba watu hao waliuawa katika eneo hilo baada ya kutokea kwa mapambano makali kati ya waandamanaji na Askari Polisi.

Mbali na mauaji hayo pia kumetokea uharibifu mkubwa wa mali katika eneo hilo ambapo ofisi  za serikali zimevamiwa na kuchomwa moto huku daraja la Mikindani nalo likivamiwa na kuvunjwa ili kuzuia mawasiliano pamoja mwingiliano wa watu kutoka Mtwara mjini kuingia eneo hilo.

"Mapambano ni makali katika eneo la Shangani huku waandamanaji hao wakielekea kwenye nyumba za vigogo zilizopo jirani na eneo mapigano kwa sasa, hivi tunavyozungumza tumehifadhiwa katika Kanisa moja hapa maeneo ya sokoni, na kuna nyumba moja ya kulala wageni (Shengena Lodge) pia imechomwa moto kwa madai kwamba iliwalaza Askari Polisi walioingia hapa Mtwara tangu juzi kwa ajili ya kuthibiti machafuko, hali ni mbaya milio ya risasi na mabomu ndiyo yanayosikika"alisema Mwandishi wa Habarimpya.com.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa