Home » » PICHA:Cheki jinsi Polisi Walivyowatawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake na Kuchoma Moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani. huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani

PICHA:Cheki jinsi Polisi Walivyowatawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake na Kuchoma Moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani. huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani


Askari
wa kutuliza ghasia




Diwani Chehako akiwa nyumbani kwake
mahakama ya Mwanzo


Mwandishi wa Channel Ten, John Kasembe
 

 Askari
wa kutuliza ghasia wakijiandaa kuzuia vurugu zilizotokea Mtwara, jana kwa kile kilinachodaiwa ni mwendelezo wa vurugu za madai ya gesi.
---
POLISI jana wamelazimika
kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika kata ya Chikongola, Manispaa
ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani
wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya
nyumba yake, huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa.



Habari
ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, Maria Nzuki
zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni
wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na
kuanza kutembeza mkong’oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hilo.



Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuwasiliana na kamanda Nzuki kwa njia ya simu za mkononi hakuweza kupatikana.



Wananchi
walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake
ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwake maeneo ya
makaburi Msafa.



Wananchi walijikusanya nyumbani kwa Diwani huyo
na kumshinikiza awatoe wachawi nje ili waweze kuwadhibu, amri
iliyopingwa na Diwani huyo. Kadiri mda ulivyokwenda ndivyo wananchi
walivyozidi kuongezeka na hatimaye kulijitokeza kundi la watu walioanza
kutia vurugu, hali iliyomlazimu Chehako kuomba msaada wa polisi.



Mashuhuda
wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi walipofika
waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake zilikuwa
zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.



Chenako akihojiwa nyumbani kwake alisema:
Wananchi
waliendelea kupinga na kudai ndani ya nyumba kuna rubani na abiria wa
ndege nimewahifadhi…polisi wakawachagua wananchi watano na kuingia ndani
ya nyumba kuwasaka watu hao…hawakuona kitu, walitoka nje na kuwamabia
wenzao hata hivyo wenzao walibisha.



Walianza kurusha mawe
nyumba… polisi walianza kupambana nao kwa kuwarushia mabomu…hata hivyo
wananchi walikuwa wanakimbia na kwenda upande wapili kufanya vurugu.
Chehako
alibainisha kuwa ni kawada yake kuamka alfajiri kwa ajili ya sala ya
asubuhi, lakini asubuhi ya jana alishindwa kuamka mapema, hata hivyo
hakuweza kuhisi jambo lolote.
Ilipofika
saa 12 asubuhi nikaanza kusikia watu wakishangaa kitu nje, nilipotoka
nikakuta nyungo na tunguri ndani yake…mara wakaja vijana wawili na
pikipiki wakachukua ule ungo na kukimbia nao…nikawatuma vijana wawafuate
waurudishe…walifanikiwa na nyungo ile ilirejeshwa nyumbani hapa na
ndipo nilipouteketeza kwa moto.



Nilidhani yatakuwa yameisha,
lakini wananchi waliendelea kudai nimewafungia wahuska ndani, si kweli
hakuna mtu humu ndani wala mimi sijui kilichotokea hadi hivyo vitu
vikawa humu ndani.
Katika
mapambano hayo ya wananchi na polisi, wananchi kwa kutumia mawe
wamemjeruhi Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani hapa, John Kasembe
kwa jiwe kichwani, sehemu za kisogoni ambapo ametibiwa zahanati ya
Fajima na anaendelea vizuri.



Kwa mujibu wa Kasembe, alipigwa mawe kichwani akiwa kazini kukusanya habari na wananchi waliokuwa wakiwarushia mawe polisi.



Ofisa
wa polisi ambaye jina lake hakutaka litajwe kwa sababu si msemaji wa
jeshi hilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa gari
moja ya polisi PT 1421 limevunjwa kioo cha mbele kwa mawe.



Hadi
saa 10.00 jioni bado polisi walikuwa wanaendelea kupiga mabomu ya
machozi hewani huku wananchi wakionekana kujipanga katika makundi hali
iliyotishia usalama wa maeneo hayo.






Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za
waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani
(Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.

Wakiwa katika
mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba
mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha
Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi.

Baadhi ya barabara za mji huo zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.Kwa Habari zaidi Bofya Hapa na Hapa.......>>>

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa