Home » » MKUTANO WA WADAU WA KARANGA NALIENDELE MTWARA, WAKULIMA WASHAURIWA KUTUMIA KANUNI BORA ZA KILIMO

MKUTANO WA WADAU WA KARANGA NALIENDELE MTWARA, WAKULIMA WASHAURIWA KUTUMIA KANUNI BORA ZA KILIMO

Na Godwin Msalichuma, Mtwara

WADAU wa kilimo cha karanga Mkoani hapa wameshauriwa kutumia kanuni bora za kilimo na uvunaji wake ili kupunguza athari za maambukizi na kuenea kwa sumu kuvu (aflatoxin) ili kuongeza mauzo katika soko la ndani na nje ya nchi.

Ushauri huo ulitolewa na mtafiti wa mbegu za mafuta Dkt. Shomari Mponda wa kituo cha Utafiti wa mbegu za kilimo na mifugo cha Naliendele Mkoani Mtwara katika kikao cha wadau wa zao la karanga kilichofanyika hivi karibuni kituoni hapo.

Alisema tatizo la sumu kuvu lipo katika mazao mbalimbali ya nafaka kama mahindi, muhogo, karanga na mtama, lakini katika karanga hukumbwa zaidi kwasababu uzalishwaji wake huanzia katika udongo pale mkulima atakapofanya uzembe kipindi cha kukalibia mavuno na kama kuna dalili za ukame tatizo huwa kubwa.

Hata hivyo aliwashauri kuwa kama kutakuwa na dalili za ukame wakulima wanapaswa kunyanyulia udongo katika mashina ya mikaranga ili kutunza unyevu kuzuia zisiweze kupasuka zikiwa ardhini kwani huko ndiko kuna vimelea vya sumu hiyo ambavyo husababishwa na aina fulani za uyoga.

Alishauri njia zingine za kukabiliana na sumu hiyo ni kukausha vizuri karanga baada ya kuvunwa ili kupunguza unyevu ambao mara nyingi husababisha ueneaji wa athari hizo, vilevile kuzitunza katika majunia yanayopitisha hewa vizuri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Elly Kafiriti alisema kuwa ni muhimu wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo na uvunaji wa karanga kwani wasipofanya hivyo maambukiza ya sumu kuvu ni hatari kwa afya za watumiaji wake kwani kwa watoto wadogo huathiri ukuaji wao, huleta utindio wa ubongo na jinsi unavyokua kuanzia miaka 35 na kuendelea huleta saratani ya ini na kuongeza kuwa:

Inaathiri soko letu la nje kwa kuzirudisha karanga zetu au kutoa fedha kidogo ambazo huwa ni hasara kubwa kwa wakulima na nchi kwa ujumla, hivyo amewaomba wakulima na wadau wa zao la karanga kuwa makini katika kuvuna na kuziandaa kwa ajili ya matumizi na biashara ya zao hilo ndani na nje ya nchi.

2 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa